MZUNGUKO wa tatu wa Ligi ya wanawake maarufu kama Serengeti Lite Women's Premier League unaendelea na leo kutakuwa na mpambano mkali kati ya Yanga Pricincess dhidi ya Tanzanite SC utakaochezwa Uwanja wa Karume.
Yanga wanaingia Uwanjani wakiwa wamefanikiwa kupata ushindi wa mchezo wao mmoja kati ya miwili waliyocheza huku wapinzani wao Tanzanite wakiwa wamepoteza michezo yote miwili waliyocheza mpaka sasa.
Jumla ya timu 12 za wanawake zinashiriki mashindano haya huku bingwa mtetezi wa kombe la ligi ya wanawake ni JKT Queens ambaye alichukua msimu uliopita.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Cliford Ndimbo amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kutoa sapoti za kutosha kwani mpaka sasa mwamko wao umekuwa mdogo.
"Mashabiki na wadau wanapaswa watambue kwamba ligi ya wanawake ina msisimko wa kipekee, wanapaswa wajitokeze kwa wingi ili kuwapa sapoti wachezaji pamoja na kuona namna Tanzania ilivyobarikiwa vipaji vya aina yake," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment