MMOJA SIMBA KUSEPA ZAKE MAJUU
Imeelezwa kuwa kiungo wa klabu ya Simba SC, Said Ndemla, anatarajia kuondoka siku yoyote kuanzia leo kuelekea nchini Sweden.
Taarifa imesema Ndemla ataondoka kuelekea nchini humo kufanya majaribio na AFC Eskilstuna.
Ndemla alishawahi kufanya majaribio katika klabu hiyo na kufuzu ila hakuweza kujiunga nayo na sasa Eskilstuna wanataka kumfanyia majaribio mengine kujua kama yupo fiti.
Kiungo huyo mshambuliaji mwenye sifa ya kufunga mabao nje ya 18 anaweza akawa moja ya wachezaji wa kulipwa ambao wanacheza soka nje ya nchi.
Nikimuangalia Ndemla naona safari hii ndio basi tena ajiandae na maisha ya baridi ya ulaya. Kwanza physical fitness ya Ndemla imeimarika sana na ni moja ya sifa ya wachezaji wa ulaya. Hata physical structure ya Ndemla ipo tofauti hivi sasa anaonekana kujengeka zaidi kimwili. kufeli ni maaumuzi yake mwenyewe Ndemla kwani anatoka kwenye timu yenye ushindani vile vile anatakiwa kufahamu yakwamba kinachotafutwa na wengi mara nyingi kupatikana sio rahisi lazima ujitoe na ukipata nafasi basi usizembee.
ReplyDelete