January 13, 2019



KIKOSI cha Simba Queens kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Yanga Pricness katika mchezo wa Ligi ya Wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Women's Premier League uliochezwa Uwanja wa Karume.

Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa ushindani mkubwa na ni kwa mara yya kwanza wanakutana kwenye mchezo huu kutokana na Yanga Princess kupanda msimu huu.

Mabao ya Simba Queens yalifungwa Amina Ramadhani bao 1, Mwanahamis Omari mabao 4, Frola Kayanda mabao alijifunga 1 na Amina Ally 1.

Simba Queens wanafikisha pointi 13 baada ya kucheza michezo mitano wakiwa nafasi ya pili huku Yanga Princess wakiwa nafasi ya saba baada ya kucheza michezo mitano wakiwa na pointi sita na kinara ni JKT Queens mwenye pointi 15.

3 COMMENTS:

  1. Duuuuuuuuuh, kumbe simba ni simba tu hata jike naye ni simba?

    ReplyDelete
  2. wana mabinti warembo mno,nitakuja kuwaona na kuwapatia vizawadi japo sio mpenzi wa simba

    ReplyDelete
  3. Hawafanani ni mitulinge ya jangwani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic