January 24, 2019




Kocha wa zamani wa Simba, Dragan Popadic ambaye kwa sasa yupo Singida United akiwa na kandarasi ya miezi sita anapata taabu sana kwa kushindwa kuambulia matokeo katika michezo yake miwili aliyoongoza mpaka sasa.


Popadic alikabidhiwa mikoba na uongozi wa Singida United akimpokea Hemed Morocco ambaye kwa sasa yupo na kikosi cha timu ya Taifa cha vijana.


Katika masharti aliyopewa ilikuwa ni pamoja na kufanikisha timu kuleta ushindani kwenye mashindano ya SportPesa Cup, mambo yamekuwa kinyume na ameaga mashindano katika hatua ya kwanza.


Singida United walitolewa kwenye hatua ya robo fainali ya kombe la SportPesa na kikosi cha Bandari kwa kufungwa bao 1-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.


Pia katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara mzungu wa Singida alikubali kupoteza mchezo wake wa kwanza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mbao na kumfanya ashindwe kupata matokeo katika michezo yake miwili ya mwanzo.

3 COMMENTS:

  1. Mjadala mkubwa unatakiwa kulinusuru Soka la Tanzania....kuanzia TFF Bodi ya Ligi kuna yafuatayo ambayo yanaua soka
    1. Ubadhirifu wa Pesa,Wizi, madeal ya wajanja wajanja katika kuuza na kuingia mikataba ya jezi na Matumizi mabovu ya pesa (Vyama vya Soka mpaka Klabu)
    2. Rushwa katika Waaamuzi wa Soka ngazi zote
    3. Upangaji mbovu wa Ratiba za Michezo ya Ligi huku baadhi ya timu zikipewa upendeleo maalumu kwa sababu ya upenzi wa Baadhi ya Viongozi wa Soka
    4. Kutokuwa udhamini wa mashindano, hakuna sera na viongozi wenye weledi na wanaojua kutafuta vyanzo vya mapato na masoko kwaajili kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa timu za mpira wa miguu
    5. Hakuna ushirikiano wenye tija kati ya TFF na vilabu vyote....baadhi ya vilabu hasa vya Dar Es Salaam kupata "preferential treatment" over others....

    ReplyDelete
  2. Why kichwa cha Habari kocha wa simba na ndani Kocha wa singida

    ReplyDelete
  3. Ujinga tu.Kocha wa Simba ni Patrick Aussems.Hawa makanjanja wanataka cheap publicity hawajui wanajiharibia.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic