BAADA ya Azam FC kufikisha pointi 47 wakiwa wamecheza michezo 20 sawa na Yanga ambao wana Pointi 53 wakiwa nafasi ya kwanza kocha wa Azam FC amejipa matumaini ya kuwa nafasi ya kwanza iliyo mikononi mwa Yanga.
Hans Pluijm amesema kikosi chake kinacheza kwa hesabu kali hali inayofanya kipate matokeo katika michezo yake hivyo ni suala la wakati kushika nafasi ya kwanza.
"Kwenye mpira kila kitu kinawezekana kikubwa ni mipango na hesabu, hakuna haja ya kuwa na hofu kama una kikosi kizuri na kinapata matokeo suala la nafasi ni muda tu.
"Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo hivyo ni wakati wetu kutafuta matokeo kwa nidhamu tukiwa ndani ya Uwanja kupitia hayo tutaushangaza ulimwengu wa mpira kama ilivyo kwa sasa, nachofurahia ni kupata matokeo chanya na ni jambo linalotufarahisha wote ndani ya timu," alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment