SIMBA WAMVAA MBELGIJI AUSSEMS
Kufuatia kichapo cha maao 2-1 kutoka kwa Bandari FC ya Kenya kwenye mchezo wa SportPesa CUP, mashabiki wa Simba wamemtupia lawama Kocha Mkuu, Patrick Aussems.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya kuondolewa kwenye mashindano hayo na kuifanya Bandari iweze kutinga hatua ya fainali kucheza na Karibangi Sharks ya Kenya pia.
Mashabiki hao wamelalama kuwa Mbegiji Aussems alipanga kikosi ambacho hakikuwa na madhara haswa baada ya kukifanyia mabadiliko kunako kipindi cha pili.
Wameeleza kwa hasira kuwa Mbelgiji huyo ameshindwa kukipa nafasi kilichoanza kipindi cha kwanza vema na kupelekea mabadiliko ambayo yalikuja kuiathiri timu.
Aidha, mashabiki hawakusita kutuma salaam kwa viongozi wa Simba kwa kuwatak waache kuyachukulia dharau mashindano haya ambayo yanafanyik kwa mara ya tatu sasa.
Fainali ya mashindano itafanyika Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Bandari watacheza na ndugu zao Bandari FC.








0 COMMENTS:
Post a Comment