SIMBA WATOA TAMKO KUHUSIANA NA WACHEZAJI 7 WALIOTOROKA KWENDA KLABU USIKU
Baada ya lile sakata la wachezaji takribani 7 wa Simba kutoroka kambini na kuelekea klabu usiku kabla ya mechi kuelekea na Bandari FC, Ofisa Habari wa Simba amesema hana mamlaka ya kuzungumzia suala hilo.
Kabla ya mchezo na Badadari wiki jana, wachezaji Hassan Dilunga, Jonas Mkude, Sergi Wawa, Mohammed Ibrahim, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin na Hatuna Niyonzima walitajwa kuelekea klabu bila ruhusa ya uongozi.
Kufuatia tukio hilo, Manara leo asubuhi akizungumza na Maulid Kitenge kupitia kipindi cha Sport Headquartes alisema suala hilo halina mamlaka ya yeye kulitolea ufafanuzi.
Manara alisema kweli yeye ndiye Ofisa mtoa habari ndani ya Simba japo hilo suala akieleza lina watu wengine walio juu yake wanaweza kuzungumzia.
"Unajua mimi sina mamlaka ya kulizungumzia suala hilo, sina mamlaka, kunwa wengine ambao wanaweza kulisemea" alisema.
Wakati sakata hilo likizi kushika kasi zaidi, kikosi cha Simba kinatarajiwa kukwea pipa kesho Jumanne kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.
Leo Hii msemaji wa Simba Hana Mamlaka ya Kuzungumzia Swala kama Hili linalohusu Wachezaji wa Simba na status ya Simba Kama Klabu Kubwa!!!
ReplyDeleteUkistaajabu ya Musa Utataona ya Firauni
WALE WOTE WANAOIHUJUMU YANGA KUANZIA KWENYE USAJILI KUVURUGA UCHAGUZI WA YANGA KIZUNGUMKUTI, TFF RATIBA KUPANGULIWA KWA KUIUMIZA YANGA, NA HILA ZOTE KWA SUALA LA BENO KAKOLANYA, .......LAANA YAKE NI MPIRA WA TANZANIA KUFA, KUFUNGIWA NA FIFA, SIMBA KUONDOLEWA CAF CL, KUKOSA UDHAMINI WA LIGI, TIMU ZA TANZANIA KUTOLEWA FAINALI ZA SPORTSPESA ...NA MAMBO MENGI KUTOKWENDA VIZURI.....CHANZO NI DHAMBI YA KUIHUJUMU
ReplyDeleteMsemaji wa club mpaka apewe mamlaka na wakuu ndo atoe hyo habar kama hajamwambia yeye atasema nn? hv ninyi mnaijua protocally ya uongozi au mnazungumza tu
ReplyDelete