IDADI HII SIMBA KUWAFUATA WAARABU KESHO
Msafara wa klabu ya Simba ukiwa na wachezaji 20, benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi unaondoka nchini kesho jioni (29/01/2019) kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.
Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa timu hiyo Haji Manara imeeleza kuwa msafara huo utapitia Addis Ababa nchini Ethiopia na kisha kuelekea Mjini Alexandria nchini Misri ambako mchezo huo utachezwa siku ya Jumamosi ijayo tarehe 2, Februari, 2019.
Simba wanaenda kukipiga na waarabu wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 5-0 dhidi ya AS Vita ya Congo katika mechi iliyopita.
Katika hatua nyingine uongozi wa klabu hiyo umemteua Patrick Rweyemamu kuwa Meneja wa muda wa timu huku aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Abbas Ally akitakiwa kuendelea na majukumu yake ya awali kama mratibu wa timu.
WALE WOTE WANAOIHUJUMU YANGA KUANZIA KWENYE USAJILI KUVURUGA UCHAGUZI WA YANGA KIZUNGUMKUTI, TFF RATIBA KUPANGULIWA KWA KUIUMIZA YANGA, NA HILA ZOTE KWA SUALA LA BENO KAKOLANYA, .......LAANA YAKE NI MPIRA WA TANZANIA KUFA, KUFUNGIWA NA FIFA, SIMBA KUONDOLEWA CAF CL, KUKOSA UDHAMINI WA LIGI, TIMU ZA TANZANIA KUTOLEWA FAINALI ZA SPORTSPESA ...NA MAMBO MENGI KUTOKWENDA VIZURI.....CHANZO NI DHAMBI YA KUIHUJUMU
ReplyDelete