SIMBA YAPEWA ONYO NA TAHADHARI
Wakati kikosi cha wekundu wa Msimbazi Simba kikikwea pipa jana kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Haki za Wachezaji (SPUTANZA), Mussa Kisoki, ametoa neno lake.
Kisoki amewapa tahadhari Simba kuhakikisha wanaimarisha umoja na mshikamano watakapofika Misri ambapo wikiendi hii watacheza dhidi ya Al Ahly kwenye kipute hicho cha kundi D.
Mwenyekiti huyo amesema Simba wanatakiwa kushirikiana kwa kila kitu kwa kile watakachokuwa wanakifanya ili kuepuka fitina za Waarabu ambao wamekuwa wazuri kucheza mechi nje ya uwanja,
Amesihi kwa kusisitiza kuwa hilo wanapaswa kulizingatia kuepusha kumaliza mechi kabla ya dakika 90 ndani ya uwanja akisema waraabu wapo vizuri zaidi kuharibu mambo nje ya kapeti.
"Nawasihi Simba watakapowasili Misri wawe makini zaidi ili kuepuka fitina za waarabu, wajaribu kushirikiana kwa kila kitu, kama kula waende pamoja ili wasije kufanyia mabaya na wapinzani wao kwa maana wamekuwa wazoefu wa kuzoofisha haswa katika mashindano kama haya" alisema.
Asante sana Muheshimiwa kwa ushauri wako.
ReplyDelete