January 27, 2019


Kiungo mjanja ambaye usajili wake uliteka vichwa vya habari hapa nchini, Feisal Salum 'Fei Toto' amesema anafurahia kucheza na mkongwe, Haruna Moshi 'Boban'

Toto ameeleza kuwa ukongwe wa Boban unasaidia kumpa uzoefu wa vitu mbalimbali ikiwemo utulivu anaouonesha mkongwe huyo uwanjani.

Amefunguka kwa kusema si jambo hata kidogo kucheza na mtu kama yule kwani ana vitu vingi ambavyo yeye kama chipukizi hana kwa sasa.

Amemtaja Boban kuwa mchezaji anayempa majukumu tofauti akicheza naye pamoja ndani ya kikosi na vilevile hupata majukumu mengine anapocheza na Tshishimbi.

"Kucheza pamoja na Boban si jambo dogo, ni mchezaji mwenye uzoefu anayenifunza vitu vingi haswa kwenye safu ya kiungo. Ana utulivu na mwenye kipaji cha aina yake akiwa analisakata gozi" alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic