January 28, 2019


JanaJumapili, fainali ya michuano ya SportPesa Cup ilifanyika katika ardhi ya Tanzania huku timu zilizoshindania kombe zote zikiwa ni KK Sharks na Bandari na zote ni kutoka Kenya. Ni aibu kwelikweli, lakini ndiyo soka ilivyo.

Michuano hiyo ilikuwa na timu nane nne zilikuwa kutoka Tanzania na nne kutoka Kenya ni msimu wake wa tatu kufanyika na leo inakuwa mara ya pili kuchezwa Uwanja wa Taifa, ilianza mwaka 2017 tulishuhudia fainali Kati ya Gor Mahia na AFC Leopards mwaka 2018 ikafanyika Kenya fainali ilikuwa ni Simba na Gor Mahia na leo ni fainali kati ya Bandari na KK Sharks zote za Kenya.

Awali timu shiriki kutoka Tanzania zilikuwa ni Singida United, Yanga, Simba na Mbao huku zile za Kenya ikiwa ni pamoja na Bandari, Gor Mahia, AFC Leopards na KK Sharks.

ZILIKOTOKA

Timu zote zilianza na hatua ya robo fainali ambapo Jumanne Uwanja wa Taifa mashindano yalianza na maumivu Kwa timu za Tanzania ambapo saa 8:00 Singida United walianza kutolewa na Bandari Kwa kufungwa bao 1-0 lilifungwa Kwa adhabu ya penalti.

Kabla mashabiki wa Singida United hawajapoa msiba mwingine ukawa Kwa kwelikweli! Yanga ambao walitolewa na KK Sharks Kwa kufungwa mabao 3-2.

MBAO SHUJAA

Wakati mzigo mzito ukiwa Kwa Mbao hatua ya robo fainali walivunja rekodi iliyodumu miaka miwili Kwa Gor Mahia kutofungwa ndani ya dakika 90 na kutwaa ubingwa mara mbili mfululizo Mbao walianza kufungwa ndani ya dakika 90 na walisawazisha bao walilofungwa kwa mkwaju wa Penalti na kufanya dakika 90 kukamilika kwa Sare ya bao 1-1.

Waliwatoa Mabingwa watetezi kwa penalti 4-3 hali ambayo imewafanya wawe mashujaa Kwa kuwa ni msimu wao wa kwanza kushiriki na wamewavua ubingwa Gor Mahia.

NIDHAMU MBOVU TIMU ZA BONGO

Kenya wamezikamata timu za Bongo na kuzichezesha namna zinavyotaka kutokana na hilo.

Mabao mengi ya ushindi Kwa timu za Kenya yametokana na adhabu walizopata.

Singida United walitolewa hatua ya robo fainali na Bandari kwa bao moja lililofungwa Kwa mkwaju wa Penalti.

Bao la Simba la kusawazisha mchezo wa nusu fainali ilikuwa ni penalti huku timu zote za Tanzania hakuna aliyepiga penalti ndani ya dakika 90.

KUPUUZIA MASHINDANO

Timu kubwa Yanga na Simba hakuna timu iliyokuwa imewekeza nguvu kubwa kwenye mashindano kila mmoja alishiriki ilimradi akamilishe ratiba hali ambayo imeruhusu haya yote yatokee.

Kwa mfano Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema wachezaji wake walipoteza umakini kutokana na kuchoka hii inamaanisha hawakuhitaji kushiriki Ila kwa kuwa ni mashindano ya mdhamini wao ikawa bora liende.

Hata Kwa Kocha wa Simba, Patrick Aussems yeye alisema kombe hili sio mpango wake kushiriki haoni umuhimu wake anashiriki kuandaa kikosi kimataifa.

WACHEZAJI KUKOSA MORALI YA KUPAMBANA.

Timu za Tanzania zilikuwa zinacheza kipindi kimoja Kwa mfano Yanga kipindi cha Kwanza aliamini ni mchezo wa kirafiki akashtuka kipindi cha pili akaambulia mabao mawili.

Simba wachezaji walijituma kipindi cha kwanza na walipata bao kwenye mchezo wao wa nusu fainali ila wakapoteana kipindi cha pili wakaruhusu mabao mawili yaliyowatoa kwenye mstari.

WAAMUZI WALIZINGUA

Umakini wa waamuzi wa mashindano haya kwa hatua ya robo fainali na nusu fainali ilikuwa ni mauza uza kwani maamuzi yao yalikuwa ni ya mashaka, kwa mfano katika mchezo wa robo fainali kati ya Simba na AFC Leopards mwamuzi alimwonyesha kadi tatu mchezaji wa Simba Claytous Chama kwa kosa ambalo lilikuwa ni la kawaida, alianza kumuonyesha kadi ya njano akamuonyesha nyekundu kabla ya kuifuta na kumuonyesha kadi ya njano jambo linaloonyesha kwamba mawasiliano kwa waamuzi yalikuwa hafifu.

TIMU ZA BONGO KUPISHANA NA FUKO LA HELA

Mshindi wa mashindano haya leo mbali na kupewa kombe atakabidhiwa zawadi ya dola 30,000 mkwanja ambao kama Yanga na Simba wangekomaa wangweutengeneza ndani ya siku saba kuliko kukomaa sana kwenye Ligi abayo mpaka sasa bado haijajulikana zawadi ya Bingwa ni nini.

BATA LA KWENDA ULAYA NA KUCHEZA NA EVERTON ITABAKI STORY

Mshindi ana bahati nyingine ya kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Everton ambayo inashiriki Ligi Kuu England hali ambayo inazifanya timu za Tanzania kuishia kusikia kwenye bomba kwani kwa misimu yote mitatu fursa hii imekuwa kwa wakenya.

FUNZO KWA TIMU WANAUABISHA UWANJA WA TAIFA

Timu za Tanzania zinapaswa zitambue kwamba kila mara zinaposhiriki michuano hii zinapaswa zijipange zisiruhusu kudharaulika kiuwezo kwani ni mara ya pili sasa kombe linatoka katika ardhi ya Tanzania na kwenda Kenya hii sio sawa inabidi iwe ni funzo kwa timu zetu.

UBOVU WA RATIBA ZA MASHINDANO

Wakati huu pia waandaaji wanapaswa waangalie kwamba ni namna gani ya kuaanda michuano hii ili iweze kwenda sawa na ratiba za michezo mingine kuwapa nafasi walimu kujipanga kutumia kikosi chao bila kuwa na hofu kama wengi walivyokuwa wakieleza.

Michuano hiyo ilimalzika jana kwa Kariobangi Sharks kuibuka mshindi baada ya kuilaza Bandari FC kwa bao 1-0 huku Simba naye akishika nafasi ya tatu kwa ushindi wa bao 5-3 zilizopatikana kwa matuta baada ya dakika 90 kwenda 0-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic