January 29, 2019


Wakati wapenzi, mashabiki na wanachama wa Yanga wakisubiri kwa hamu uchaguzi wa kujaza nafasi ndani ya klabu hiyo, bado mpaka sasa haijaelewa utafanyika lini.

Taarifa zinaeleza mpaka sasa haijajulikana ni lini utafanyika kufuatia ukimya ambao upo na inasemekana wanachama waliofungua kesi mahakamani hawajafuta kesi zao.

Wanachama baadhi walifungua kesi kupinga kufanyika kufanyika kwa uchaguzi huo na lakini baadaye baadhi ya viongozi Yanga waliwashawishi kuzifuta japo imekuwa ngumu.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Ally Mchungahela, alisema wanazungumza vema na wanachama hao kuhakikisha wanafuta kesi zao na akaeleza maendeleo ni mazuri.

Uchaguzi wa Yanga ulipaswa kufanyika tarehe 13 mwezi huu wa kwanza lakini mpaka sasa umeshindika na leo ikiwa ni tarehe 29 kuelekea mwisho wa mwezi bado haijajulikana hatma ni nini.

1 COMMENTS:

  1. WALE WOTE WANAOIHUJUMU YANGA KUANZIA KWENYE USAJILI KUVURUGA UCHAGUZI WA YANGA KIZUNGUMKUTI, TFF RATIBA KUPANGULIWA KWA KUIUMIZA YANGA, NA HILA ZOTE KWA SUALA LA BENO KAKOLANYA, .......LAANA YAKE NI MPIRA WA TANZANIA KUFA, KUFUNGIWA NA FIFA, SIMBA KUONDOLEWA CAF CL, KUKOSA UDHAMINI WA LIGI, TIMU ZA TANZANIA KUTOLEWA FAINALI ZA SPORTSPESA ...NA MAMBO MENGI KUTOKWENDA VIZURI.....CHANZO NI DHAMBI YA KUIHUJUMU

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic