Mshambuliaji mpya wa Cardiff City, Emiliano Sala alituma ujumbe mfupi kupitia kundi la whatsapp muda mfupi kabla ya kupanda ndege ambayo baadaye inaelezwa kuanguka.
Bado juhudi zinafanyika kuhakikisha ndege hiyo inapatikana ingawa inaonekana matumaini ya kumpata akiwa mzima, yamepungua kwa asilimia 90.
Emiliano aliyekuwa akirejea Cardiff kuanza kazi baada ya kununuliwa kwa pauni million 15 akitokea Nantes ya Ufaransa, hajapatikana leo ni siku ya tatu.
Katika ujumbe huo, Sala alikuwa akiwaeleza namna alivyokuwa na kazi nyingi akijiandaa kutoka Nantes kwenda Cardiff huku akionyesha kuwa na hofu ya ndege atakayoipanda.
Mashabiki mjini Nantes wameendelea kukusanyika wakiwa na maua huku wakiimba nyimbo kuhusiana na mchezaji huyo raia wa Argentina.
0 COMMENTS:
Post a Comment