KIKOSI cha Yanga Princess leo kimeibuka na ushindi mnono mbele ya kikosi cha Mapinduzi Queens katika mchezo wa Ligi ya Wanawake maarufu kama Serengeti Lite Women's League uliochezwa Uwanja wa Karume.
Yanga Princess walianza kwa kasi katika mchezo wa leo na kipindi cha kwanza walifunga kupitia kwa Thadei Aidan dakika ya nane na dakika ya 11 Fausta Thomas akaandika bao la pili, Aisha Juma dakika ya 22 bao la tatu kabla ya Thadei Aidan kufunga bao la nne dakika ya 25.
Kipindi cha pili Yanga waliendelea kasi yao ya kushambulia na walipata bao la nne dakika ya 90 Fausta Thomas alifunga mabao mawili na kufanya Yanga washinde kwa mabao sita huku Mapinduzi Queen wakiambulia patupu leo.
0 COMMENTS:
Post a Comment