January 7, 2019


Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema hatatengua uamuzi wake wa kumvua unahodha Kelvin Yondan licha ya baadhi ya mashabiki kuanza kuhoji uamuzi huo, kwa madai kuwa unaweza kuigawa timu hiyo.

Kocha huyo mwenye uraia wa DR Congo na Ufaransa, alisema kwamba wakati anaanza kukinoa kikosi hicho alionekana kugombana na Ajibu juu ya nidhamu lakini amejirekebisha kwa kiasi kikubwa na sasa ni mfano wa kuigwa.

Yondani alivuliwa unahodha na kocha wake baada ya kukosa mazoezini bila taarifa kitendo ambacho kilimfanya kocha wake kuchukua uamuzi wa kumwondoa katika uongozi na kumpa Ibrahim Ajib, awali Yondan alikuwa nahodha msaidizi lakini baada ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kustaafu akawa nahodha mkuu akisaidiwa na Juma Abdul ambaye ni swahiba wake mkubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic