A-Z NAMNA YANGA ILIVYOVUNJA MWIKO CCM KIRUMBA
TANGU ipande daraja timu ya soka ya Mbao FC ilikuwa haijawahi kufungwa na Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba wa jijini hapa, lakini juzi kwa mara ya kwanza ilipata kichapo kikali.
Mbao FC ilipata kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga katika mchezo huo uliokuwa wa vuta nikuvute uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Championi Ijumaa ambalo lililokuwepo uwanjani hapo linakuletea baadhi ya mambo ambayo yalitokea kabla na baada ya mchezo huo.
Matokeo hayo yaliifanya Yanga kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa na jumla ya pointi 61 baada ya michezo 25.
YANGA WAKATIZA UWANJANI
Yanga waliingia kwenye Uwanja wa CCM Kirumba majira ya saa 8:50 mchana na baada ya kuingia uwanjani gari aina ya Costa iliyokuwa imewabeba, ilipaki pembezoni mwa uwanja na kushuhudia wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi la Yanga w a k i ingia uwanjani kwa kupi- t a katikati ya mstari unaotenganisha dimba na kuingia vyumbani moja kwa moja.
IMANI ZA KISHIRIKINA ZATAWALA
Katika mchezo wa Mbao FC dhidi ya Yanga imani za kishirikina zilitawala zaidi mchezo huo, kwani gazeti hili lilikuwepo uwanjani hapo lilishuhudia wachezaji wa timu ya Mbao FC wakiwa wa kwanza kuingia uwanjani kupasha misuli.
Baada ya kuingia walienda eneo la Kusini mwa uwanja huo na kuzunguka kibendera kisha upande wa Kaskazini na kuzunguka tena kibendera, hali hiyo pia ilitokea kwa Yanga ambao nao pia walifuata njia ambazo walizifanya wachezaji wa Mbao FC wakati wanaingia uwanjani.
MBEBA CHUNGU AINGIA NA PUNDA
Mbeba Chungu maarufu wa Mbao F C k a tika mchezo huo aliingia uwanjani kwa staili ya aina yake a m b a p o dakika tatu tu baada ya mchezo kuanza shabiki huyo aliingia kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na punda hali iliyomfanya ashangiliwe zaidi na mashabiki
wa Mbao FC.
MAKAMBO AMUINUA ZAHERA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makam
bo wakati mchezo ukiendelea mchezaji huyo alimuinua kwenye benchi kocha wake mkuu, Mwinyi Zahera na
kuanza kuzungumza naye. Championi Ijumaa lilipozungumza na kocha huyo kipi alikuwa akiambiwa na Makambo alisema kuwa kuna mapungufu aliyaona, hivyo alikuwa akishauri kufanyika kwa mabadiliko ndiyo maana tulimtoa Ibrahim Ajibu na tukamuondoa Amissi Tambwe na kuingia Dante na Kaseke, hivyo hakukuwa na ziada.
WAAMUZI WAPONDWA CHUPA
Waamuzi waliochezesha mchezo huo ambao ni Ally Simba kutoka Geita ambaye alikuwa kati, akisaidiwa na Makame Mdogo, Godfrey Sakila na Daniel Warioba aliyekuwa mwamuzi wa akiba walijikuta katika wakati mgumu baada ya kumalizika kwa dakika 45, ambapo mashabiki wanaodaiwa ni wa Yanga waliokuwa upande wa Mashariki walianza kuwarushia chupa ya maji, hali hiyo ilisababisha waamuzi hao kushindwa kuingia kwenye vyumba ambapo baada ya kupata ulinzi mkali kutoka kwa Jeshi la Polisi walifanikiwa kuingia katika vyumba hivyo.
ZAHERA AVUNJA MWIKO KIRUMBA
“Kocha Mwinyi Zahera amevunja mwiko uliowashinda makocha waliopita akiwemo George Lwandamina pamoja na Hans Van Der Pluijm kwa kuifunga Mbao FC mabao 2-1, kwani makocha hao wawili waliopita hawakuwahi kupata ushindi katika mchezo dhidi ya wapinzani waho hao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
MASHABIKI WA YANGA WAVAMIA UWANJANI
“Kutokana na mashabiki wa Yanga kuwa na furaha kubwa baada ya kumalizika kwa mchezo huo walivamia uwanjani na kwenda kwa wachezaji ambapo polisi waliokuwepo hapo waliingia na kuwatawanya.
0 COMMENTS:
Post a Comment