February 22, 2019


TIMU ya soka ya wanawake ya Yanga Princess, imeongeza nguvu katika kikosi chake baada ya kufanya usajili wa wachezaji tisa kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.

Wachezaji hao waliosajiliwa ni Merry Charles, Mwapewa Mtumwa, Mwanaidi Tamba, Mwajuma Abdallah, Aziza Lugendo, Fadhila Hamadi, Rukia Hamisi, Tausi na Zainabu.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Siza Lyimo, alisema kuwa wamesajili wachezaji hao ili kuongeza nguvu kwa ajili ya kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri kwani wao bado ni wageni kwenye ligi hiyo.

‘’Sisi ni wageni kwenye ligi ya wanawake kwani ndiyo mara yetu ya kwanza kushiriki, hivyo kwa kuwa mzunguko wa kwanza hatujafanya vizuri basi tumeona ni vyema kuongeza nguvu kwa kusajili wachezaji wengine tisa ili tufanye vizuri zaidi,” alisema.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic