February 26, 2019



UONGOZI wa Alliance FC ya mkoani Mwanza umesema kuwa umejipanga kufanya maajabu mbele ya kikosi cha Yanga katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa  Alliance, James Mwafulango amesema wanawatambua wapinzani wao ubora wao ulipojificha hivyo watapambana kupata matokeo.

"Tuanatambua mchezo wetu wa kwanza tulipoteza ni muda wetu kuonyesha kwamba nasi tunaweza, na tutawafundisha soka wapinzani wetu maana tuna madarasa kabisa ambayo wachezaji hujifunza, mashabiki wajitokeze kwa wingi.

"Tiketi zitaanza kuuzwa siku ya jumamosi saa tano asubuhi kama kawaida Uwanja wa CCM Kirumba, mzunguko elfu tano na viti maalumu elfu kumi pekee huku watoto wakilipa shilingi elfu mbili na miatano," amesema Mwafulango.

2 COMMENTS:

  1. أفلام تورنت أكبر موقع عربي مختص بالأفلام الأجنبية المترجمة و المسلسلات الأجنبية ، مشاهدة وتحميل مجانا بصيغة التورنت
    افلام تورنت

    ReplyDelete
  2. و المسلسلات الأجنبية ، مشاهدة وتحميل مجانا بصيغة التورنت
    افلام تورنت

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic