BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Idd Bonge, ameibuka na kuomba radhi baada ya kufungiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC).
TPBRC ilitangaza kumfungia kwa muda usiojulikana kujihusisha na mchezo huo ikiwemo hata kuingia katika viwanja, bondia huyo katikati ya wiki iliyopita kufuatia kufanya fujo katika pambano kubwa kati ya Idd Pialali na Mmalawi, Wilson Masamba baada ya bondia wake, Wazir Rosta, kupoteza kwa pointi mbele ya Mbena Rajab.
Bonge amesema: “Ngumi kwangu ni kazi na ajira kukosea kwangu ni hasira na hali ya binadamu sikutarajia kufanya hivyo naomba msamaha ili nirejee katika kazi yangu naomba nifunguliwe na niendelee na kazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment