February 6, 2019


Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Samuel Lukumay, amewapiga mkwara mzito baadhi ya wale wanaodaiwa kupanga kuihujumu klabu, imeelezwa.

Lukumay amefunguka hayo baada ya uwepo wa tetesi zinazoelewa kuna watu wamepanga kula fedha za Yanga wakati klabu inapitia wakati mgumu.

Kauli hii si ya kwanza kutoka Yanga kwani hata baadhi ya wadau wamekuwa wakisema kuna ubadhirifu wa fedha umekuwa ukifanyika ndani ya utawala uliopo madarakani.

Taarifa imeeleza kuwa Kaimu huyo amesema endapo kuna yoyote atabainika kuhujumu chochote ndani ya Yanga atakula naye sahani moja ikiwemo kuchukua hatua za kisheria.

Hivi karibuni kumekuwa kunaelezwa kuwepo kwa baadhi ya wanachama ndani ya klabu hiyo wanaoitumia klabu kwa ajili ya kujaza matumbo yao.

1 COMMENTS:

  1. Kwani leo ndo mnatambua hilo kwa kweli watanzania tunadanganywa, hv we lukumay nn ambacho hukifahamu kuhusu upigaji wa yanga au kuridhisha wanachama acheni habarhabar bwana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic