February 26, 2019



LIPULI FC iliyo chini ya kocha Seleman Matola leo itaikaribisha Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Samora majira ya saa 10:00 jioni.

Kwenye mchezo wa leo kiinglio kitakachokupa fursa ya kuona krosi wa beki na kupanda wa Simba, Zana Coulibary na mshambuliaji matata kwa mijishuti, Haruna Shamte kwa viti vya mzunguko ni shilingi elfu tano tu 'buku tano, huku ile ya viti maalumu ikiwa ni shiling elfu kumi pekee .

Timu hizo zinakutana leo ikiwa ni mara ya nne tangu Lipuli ipande Ligi Kuu msimu wa 2017/18 na katika michezo yao yote mitatu ya nyuma hakuna aliyebeba pointi tatu.

Walipokutana Iringa Simba waliambulia sare ya kufungana bao 1-1 huku lile la Lipuli likifungwa na Adam Salamba ambaye kwa sasa yupo Simba na lile la Simba likifungwa na Laudit Mavugo ambaye kwa sasa yupo Burundi.

Mchezo wa Uwanja wa Taifa Simba walilazimsisha sare ya kufungana bao 1-1 ambapo lile la Simba lilifungwa na Mwinyi Kazimoto yupo JKT Tanzania na lile la Lipuli likifungwa na Asante Kwasi yupo Simba kwa sasa.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu huu walitoka suluhu Uwanja wa Taifa ivyo leo ni mara ya nne na wafungaji wote wa Lipuli wapo Simba kwa sasa.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic