February 12, 2019
Kikosi cha vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga kililazimika kuahirisha mazoezi mjini Morogoro ili kungalia mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba dhidi ya Al Ahly.

Katika mechi hiyo, Simba imepata ushindi wake wa pili hatua ya makundi kwa kuichapa Ahly kwa bao 1-0 lililofungwa na Meddy Kagere.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameamua kufanya utaratibu huo kama sehemu ya kuwasoma Simba kabla ya mechi yao itakayochezwa Jumamosi mjini Dar es Salaam.

Yanga ipo kambini mjini Morogoro, lakini Zahera aliamua kuahirisha mazoezi na sehemu ya programu yake ikawa ni kuwaangalia Simba.

“Kocha aliamua hiyo iwe sehemu ya programu kwa kuwa baada ya mechi hiyo, Yanga inakutana na Simba,” kilieleza chanzo.

Yanga ipo kileleni mwa Ligi Kuu Bara ikiwa ina pointi 58 baada ya kucheza mechi 23 wakati Simba ya tatu ikiwa na pointi 36 baada ya mechi 15.

4 COMMENTS:

 1. Simba haisomeki kihivyo , atakutana na kikosi kipana kikiongozwa na nyoni,niyonzima, ndemla, mo ibrahimu, rashidi juma , salamba , gyan, mlipili na wengine ambao hawajawaona na kuwasoma .this is simba , yes we can

  ReplyDelete
 2. Akaangalie sana.Hata kocha wa Al Ahly aliahirisha zoezi kuangalia kideo cha Simba na akaingia chaka.Al ahly ni ya kwanza kwa soka Afrika..na simba ya 30....Je Yanga ni ya ngapi

  ReplyDelete
 3. Kagere hasomeki .Sawa utamsoma akiwa amefumba jicho la kushoto , lakini atakugeuzia kibao kwa kufumba jicho la kulia

  ReplyDelete
 4. KAGERE NA SIMBA WALISOMEKA WALIPOPIGWA KHAMSA NA AHLY NA PIA KHAMSA NA VITA
  ACHENI TAMBO ZENU MTABAKI NA HIZO HIZO POINT SITA MAANA MTAPIGWA KULE ALGERIA NA PIA MTAPIGWA NA VITA HAPO KWA MCHINA

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV