KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema hesabu zake kwa sasa ni kwenye mchezo wake wa kesho dhidi ya Azam FC utakaochezwa Uwanja wa Samora.
Matola amesema kuwa anafurahishwa na uwezo wanaonyesha vijana wake ndani ya uwanja hali inayompa matumaini ya kupata matokeo.
"Tumemaliza habari za KMC sasa ni mwanzo mwingine kwa ajili ya kufungua ukurasa mpya wa maandalizi dhidi ya kikosi cha Azam FC, tupo tayari na tutatumia vema uwanja wetu wa nyumbani.
"Kikubwa ambacho tunahitaji ni kuona tunabaki na pointi tatu mkononi ilikuendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri, wachezaji wanatambua kwamba ligi ni ngumu nasi lazima tuonyeshe utofauti," amesema Matola.
Mchezo wa kwanza waliokutana na Azam Uwanja wa Chamazi ikiwa ni mzunguko wa kwanza waligawana pointi moja.
Lipuli inashika nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 36 baada ya kucheza michezo 24 na Azam FC wpo nafasi ya pili wakiwa na pointi 48 baada ya kucheza michezo 21.
0 COMMENTS:
Post a Comment