LIGI Kuu Bara leo imeendelea huku jumla ya timu nane zikimaliza dakika tisini na kufanya jumla ya mabao nane kufungwa leo kwenye viwanja vitatu tofauti.
Timu mbili zimepata pointi tatu huku timu mbili zikigawana pointi mojamoja kama ifuatavyo:-
Zilizochukua pointi tatu
Mwadui FC wakiwa nyumbani Uwanja wa Mwadui Complex wamebeba pointi tatu mbele ya Biashara United kwa ushindi wa mabao 2-1.
Mabao ya Mwadui FC yamefungwa na Salim Aiyee dakika ya 45 na dakika ya 64 huku lile la Biashara United likifungwa na Wazir Jr dakika ya 50 kwa mkwaju wa penalti.
Lyon wakiwa nyumbani Uwanja wa Amri Abeid wanapoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Simba.
Mabao ya Simba yamefungwa na John Bocco dakika ya 28 kwa penalti na dakika ya 46 huku bao la tatu akifunga Adam Salamba dakika ya 45.
Zilizogawana pointi mojamoja
Ruvu Shooting wamekubali kutoka suluhu nyumbani dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Mabatini.
Coastal Union wakiwa nyumbani wanalazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC.
Bao la Coastal Union lilifungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 45+2 na lile la Azam FC likifungwa na Obrey Chirwa dakika ya 52.
Ubingwa wa mwaka huu hauna ladha kwani lawama kwa bodi ya ligi ni nyingi sana timu zimezidiana michezo ya kucheza wakati wengine wana viporo 11 wengine wanaendelea kuambiwa ratiba zao lazima ziendelee....hakutapatikana bingwa bora
ReplyDeleteUBINGWA NI UBINGWA TU HAKUNA UTOFAUTI KAMA TIMU YAKO NZURI IKICHEZA MECHI ZAKE IKASHINDA TATIZO LIPO WAPI? TATIZO TUNAWEKA USHABIKI NA WOGA WA MATOKEO MABOVU. TUANGALIE MECHI ZINAZOTUHUSU TUPAMBANE TUSHINDE YA MWENZIO HAYAKUHUSU MWISHO HESABU ZITAAMUA.
DeleteSIO KWELI YANGA ILIPOFIKISHA VIPORO 4,SIMBA ILIGOMA KUENDELEA NA MICHEZO YAKE MPAKA YANGA IMALIZE VIPORO VYAKE. NA AKINA NYIE NDIO MLIPIGA KELELE SANA.SASA LEO MNAVIPOLO 11...HAIJAWAI TOKEA DUNIANI KOKOTE NI HAPA TZ TU... BODI YA LIGI WANAENDELEA KUIKAZA RATIBA YA YANGA.... KAMA SIO MIPANGO NI NINI?
DeleteThis is bcoz of frequently winning of simbaa,ha ha ha ha ha wala msijali simba hachukui ubingwa buana acheni wasiwasi.azam ndio bingwa.
ReplyDeleteThis is bcoz of frequently winning of simbaa,ha ha ha ha ha wala msijali simba hachukui ubingwa buana acheni wasiwasi.azam ndio bingwa.
ReplyDeleteThis is bcoz of frequently winning of simbaa,ha ha ha ha ha wala msijali simba hachukui ubingwa buana acheni wasiwasi.azam ndio bingwa.
ReplyDeleteViporo kila sehemu pale misri al alhly ana viporo 4. Solution ni kucheza mechi zako. Hata ukisubiri mwenzio amalize viporo lazima mwaka huu kila mtu atimize mechi 38. Hakuna atakaehukumiwa kwa mechi chache.
ReplyDelete