February 26, 2019


Klabu ya Singida United imemrejesha kocha wake wa zamani Fred Felix Minziro kwaajili ya kuimarisha benchi lake la ufundi.

Minziro atakuwa akimsaidia kocha mkuu wa timu hiyo Dragan Popadic na tayari amesafiri na kikosi kuelekea jijini Mbeya kwaajili ya mchezo dhidi ya Mbeya City.


Ikumbukwe kuwa Kocha Minziro ndiye aliyeionoza timu hiyo kuingia Ligi Kuu Tanzania Bara akiipandisha daraja msimu wa mwaka 2017/18 kabla ya kufungashiwa virago wakati timu ikianza msimu wake wa kwanza kwenye ligi kuu, nafasi yake ikichukuliwa na Hans van der Pluijm.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic