February 22, 2019





Canada, Kampuni inayokuwa kwa kasi katika masuala ya teknolojia na Burudani ya Kimataifa, SportPesa imeingia ubia katika mashindano ya magari ya Langalanga maarufu kwa jina la F1.

Mbali ya kuingia ubia, SportPesa pia itakuwa na timu ijulikanayo kwa jina la SportPesa Racing Point F1.


Tangazo la kuingia ubia katika mashindano hayo limekwenda sambamba na uzinduzi wa msimu wa awali wa mashindano hayo pamoja na gari jipya la mashindano hayo. Uzinduzi wa timu ya kwanza ulifanyika nchini Canada.


Uzinduzi huo pia ulishuhudiwa na madereva wawili maarifu, Sergio Perez na Lance Stroll, pamoja na Mkuu wa timu, Otmar Szafnauer, na Mkurugenzi wa Ufundi, Andrew Green.

Ubia huo ni wa miaka mingi na unatarajia kuleta matokeo ya haraka katika kuendeleza mchezo huo maarufu duniani wakati wote wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.


Kutokana na ushirikiano huo, magari ya Racing Point yanakuwa na rangi  ‘pink’, na BWT inaendelea kama mfadhili mkuu wa timu hiyo, pamoja na kuongezea alama ya bluu ya SportPesa kwenye mabawa ya mbele na ya nyuma, na kufunika injini.


Mkurugenzi Mtendaji wa Racing Point F1 Team, Otmar Szafnauer, alisema kuwa SportPesa ni kampuni inayokuwa na wanafaraja kubwa kuingia katika ushirikiano huo ambao unafungua ukurasa mpya katika shughuli zao za kila siku kimataifa.

“Tunafurahi kuwa na ushirikiano huu ambao utatoa ujumbe wa timu yetu na kutarajia kufanya kazi pamoja ili kuleta msisimko kwa mashabiki wa mbio za Langalanga na duniani,”


Mkurugenzi wa Kampuni SportPesa Adam Beighton alisema kuwa wana furaha kuwa sehemu ya familia ya formula One.
Beighton alisema kuwa ushirikiano huu ni muhimu sana kwao kwa sababu una watofautisha na wadau wengine katika malengo yao ya kufikia watazamaji wapya duniani.


“Tumepata jukwaa jipya linaloweza kutuwezesha kufikia dhamira yetu ya kusaidia na kuendeleza michezo ya kitaifa na kimataifa katika nchi ambazo tunafanya kazi kwa kuleta fursa mpya,” alisema Beighton.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic