Kumekuwa na shida kubwa ya utapatikanaji wa vifaa sahihi vya michezo nchini na hasa katika suala la viwango vya ubora.
Hata hivyo, wanamichezo mbalimbali wameambiwa sasa jibu la matatizo yao limepatikana baada ya kufunguliwa kwa duka kubwa maalum la vifaa vya michezo.
Wanamichezo mbalimbali wamekaribishwa katika duka jipya la vifaa vya michezo ambalo ni kubwa kuliko yote nchini.
Duka hilo la Just Fit Sports Gear lipo eneo la Makumbusho katika kituo cha mafuta cha Oil Com jijini Dar es Salaam, limefunguliwa juzi rasmi na wanamichezo wametakiwa kufika na kujipatia vifaa orijino vya michezo yote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Just Fit Sports Gear, amesema imani yake kubwa Watanzania watakuwa na nafasi kubwa ya kupata vifaa wanavyovitaka.
"Vifaa orijino imekuwa tatizo kubwa. Kwetu sasa mambo ni tofauti kwa kuwa ni uhakika na tumeingia mikataba na makampuni kadhaa ya vifaa vya michezo. Hivyo vifaa vyetu ni sahihi na orijino kabisa," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment