February 20, 2019


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera ameendelea kusisitiza kuwa kamwe hatohitaji kurejeshewa pesa zake ambazo anaisaidia timu hiyo.

Kauli ya Zahera imekuja baada ya kuwepo kwa minong'ono kutoka kwa baadhi ya wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwa ataanza kuidadi hapo baadaye.

Zahera ambaye yupo jijini Mwanza na kikosi cha Yanga kwa mechi ya ligi dhidi ya Mbao FC leo jioni, ameeleza kuwa ataendelea kujitolea kuisaidia timu ambayo inapitia wakati mgumu hivi sasa.

"Sitohitaji malipo yoyote baadaye kutoka Yanga, nimeamua kujitoa kuisaidia timu kutokana na hali ngumu inayopitia hivi sasa, nina kazi zangu zingine zinazoniingizia hela na sitegemei Yanga pekee" alisema.

Aidha, Zahera amewataka wanachama na mashabiki wa Yanga kuendelea kuichangia klabu yao kwa nguvu zote ili kuisaidia kuweka morali katika mechi zijazo za ligi.

3 COMMENTS:

  1. HATA MANJI ALITUSAIDIA SANA ZAIDI YA BILIONI 13 ALIKUWA ADAI LAKINI AKASAMEHE YANGA BANA TUNA WATU WENYE UCHUNGU NAYO HEKO ZAHERA

    ReplyDelete
    Replies
    1. nani alikuambia amesamehe?...vipi zile bilioni 11 anazodai? umesahau hadi akaomba kuikodisha klabu kwa miaka 10.

      Delete
  2. Anatetea kibarua hapo!. Kama sivyo, kuna kitu ndani yake ambacho kuja kukijua ni baadae sana. Kufikiria kirahisi tu ni hivi hii kazi ya ukocha aliichagua ili iweje! ina maana kaja Tanzania kupoteza muda na mali zake bila faida yoyote kwake?!, Je, Zahera ni Mfadhili au ni Kocha?. Mnaohusika na Yanga, mjitathimini na mchunguze kwa kina.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic