LICHA ya kutamba awali kwamba atawanyoosha Yanga ambao walikuwa wapinzani wake kwenye mchezo na matokeo yake kibao kugeuka huku akiambulia kichapo cha bao 1-0, kocha wa Alliance amesema kuwa kilichowabeba Yanga ni uzoefu.
Alliance walikaza kipindi cha kwanza hali iliyowafanya waende kwenye vyumba vya kubadilishia nguo bila kuruhusu bao wala wao kuona lango la wapinzani, ila kipindi cha pili mambo yalibadilika na kujikuta wakipoteza dakika ya 75 kwa bao la Amiss Tambwe.
Kocha mkuu, Malale Hamsini, amesema hakuwa na ujanja mbele ya wababe hao wa Ligi Kuu Bara baada ya kuzidiwa maarifa, ila bado anaamini kikosi chake kimepambana kadri ya uwezo walikosa bahati pekee.
"Niliamini nitabeba pointi tatu muhimu ukizingatia nipo nyumbani, mambo yamekwenda kombo, sababu kubwa ni uzoefu wa wapinzani wangu kwenye ligi hasa waliweza kutumia nafasi walizotengeneza huku wachezaji wangu wakishindwa kutumia makosa yao," amesema Hamsini ambaye alipoteza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Matokeo hayo yanaifanya Alliance kubaki nafasi yake ya 7 baada ya kucheza michezo 29 na pointi zake ni 36.
ReplyDeleteيلا شوت بث مباشر
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteKocha huyu angalau mtaarabu amekiri uzoefu na ukubwa wa YANGA kwa kufungwa bao 1-0 sio yule kocha wa Stand United ambaye usda mbaya inamwaminisha vibaya na hakubali kuwa alizidiwa ujanja na uzoefu na SIMBA alipofungwa 2-0 badala yake anamimina lawama kwa Refarii. wote tuliona walivyofungwa kihalali.
ReplyDeleteReplyDelete