Pamoja ya kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, AS Vita kutoka DR Congo imevunja rekodi ya Simba katika Uwanja wa Taifa kwa kupata bao moja katika kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Simba.
Wikiendi iliyopita, Simba iliandika rekodi mpya katika Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo huku ikivunja rekodi yake ya kutoruhusu bao katika mechi zake nyumbani.
Vita imevunja rekodi hiyo katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi katika Kundi D, uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa ambao ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Ipo hivi; katika mechi sita za hatua makundi, Simba imecheza mechi tatu nyumbani na tatu ugenini ambapo kwenye mechi za nyumbani walianza kwa kuifunga JS Saoura ya Algeria mabao 3-0, kisha wakaja mabingwa wa zamani wa Afrika Al Ahly nao wakachezea 1-0.
Lakini AS Vita peke yao ndiyo wamevunja rekodi hiyo kufuatia bao walilofunga juzi kwenye mchezo huo ambao umeipeleka Simba hatua robo fainali ya michuano hiyo ikiwa na pointi tisa.
0 COMMENTS:
Post a Comment