March 20, 2019


Kiungo mchezeshaji fundi Mnyar­wanda, Haruna Niyonzima ametaja siri ya kiwango chake kikubwa alichokionye­sha kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita, huku akisisitiza kwamba yeye ni yule­yule wala hajabadilika.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, juzi, Simba ilifaniki­wa kushinda mabao 2-1 huku Niyonzima akiwa gumzo kubwa.

Kiungo huyo alitokea benchi katika dakika ya 60 akichukua nafasi ya Mganda, Emmanuel Okwi na kuhusika kwenye bao la pili la ushindi lililofun­gwa na Mzambia, Clatous Chama baada ya kuu­ruka kwa makusudi mpira uliopigwa na John Bocco kabla ya bao hilo kufun­gwa.

Niyonzima alisema aliing­ia uwanjani akiwa ameona upungufu wa wapinzani wao akiwa benchi.

Niyonzima alisema, akiwa benchi kocha wake alimpa maelekezo ya nini cha kukifanya pindi aki­ingia na kikubwa alimtaka akae na mpira, kupiga pasi za kwenda mbele ili wapate bao lingine.

“Niwaambie tu watu, Niyonzima ni yuleyule wa zamani hana tofauti na huyu wa sasa, kikubwa ni nafasi tu. Nikiendelea kupata nafasi wataniona zaidi,” alisema Niyonzima.

3 COMMENTS:

  1. Kweli ndugu yangu nasi sote tumekushuhudia. Keep it up

    ReplyDelete
  2. Muda wake ulikaribia kuisha huwa anajituma sana,akishasaini contract maringo ndio yanaanza,mara harudi kwa wakati,kwenye match hajitumi wala hajali timu,tena akisaini miaka 2 hapo ndio hajali timu kabisa ni maringo tu

    ReplyDelete
  3. Na kama ni kweli muda wa näring i imekwisha Simba ni wajibu tu hamna maneno .Ukileta maneno benchi tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic