KAMATI YA FITINA SIMBA YAMALIZA KAZI ALGERIA
MTENDAJI Mkuu wa Simba, Crecentius Magori, amefunguka kuwa kamati iliyotumwa kuweka mambo sawa nchini Algeria, imekamilisha mipango na kilichobaki ni Simba kushuka uwanjani Jumamosi kufanya mambo.
Magori Alisema waliwatuma wawakilishi wawili kwenda Algeria mapema kwa lengo la kuweka mambo sawa, kubwa ikiwa ni kuunda mipango itakayoifanya Simba ivune pointi kwenye mchezo huo dhidi ya JS Saoura.
“Tulitanguliza watu mapema kule Algeria ili waandae mazingira mazuri, kitu kizuri ni kwamba ripoti waliyotuma inaonesha kuwa mambo ni shwari na suala la kupata pointi ni kubwa sana,” alisema Magori ambaye amewahi kuwa Makamu wa Rais wa TFF.
Katika hatua nyingine, beki kisiki wa Simba, Pascal Wawa amesema; “Ligi ya Mabingwa Afrika ni michuano tofauti kabisa na hii ligi tunayocheza, watu wasifi kiri kuwa mchezo utakuwa mwepesi na tutapata pointi tatu kirahisi kama tunavyofanya kwenye ligi yetu.”








NAMHESHIMU SANA BW. MAGORI, KIONGOZI WANGU, LAKINI SIZIPENDI KAULI HIZI ZISIZO NA TIJA ZA KUSEMA KAMATI YA FITNA IMEMALIZA KAZI. KWANZA SIAMINI KAMA MAGORI AMESEMA HIVYO, SIAMINI. MMESEMA HIVYO CONGO TUMEFUNGWA 5. MMESEMA HIVYO MISRI TUMELAMBWA 5. KAULI YA OVYO INADUMAZA WACHEZAJI WAKIAMINI KAULI HIZO. MPIRA NI UWEZO MPIRA NI MATAYARISHO NA KUPAMBANA UWANJANI. TUACHE KAULI ZA KUAMINISHA WACHEZAJI KUMBE WAO NDIO WANAOCHEZA UWANJANI.
ReplyDeleteUgenini ni ugenini tu hata iwe vipi na hakuna kiongozi wa fitna au kishirikina ambae anaweza kutamba kwenye klabu ya Simba yakuwa ana uwezo wa kutanzua au kung'amua mafumbo mengi ya hila linapokuja suala la fitna za kimpira barani Africa kwa nchi kama Algeria,Misri,Morocco,Tunisia,Nigeria,Congo Drc na nchi nyengine nyingi. Watanzania bado tunajifunza na fitna za kimpira barani Africa lakini inaonekana tuna uweledi au ufahamu wa mwendo wa konokono katika kujifunza huko kwani jambo moja kubwa linalotufelisha ni kutokuwa imara na wachezaji waliojengwa na mioyo ya jiwe kupambana uwanjani hasa ugenini. Simba wanaonekana wapo vizuri kwa nyumbani lakini lazima wawe makini sana kwa warabu la sivyo watapata aibu nyengine kubwa ugenini. Kwa mfano TP Mazembe alimfunga Africain ya Tunisia nane mtungi 8-0 pale Congo lakini akaenda kushindwa kupata ushindi na timu hiyo waliporejeana kule Tunisia. Kwa hivyo Simba kumfunga js Saoura tatu 3-0 hapa nyumbani kisiwe kigezo hata kidogo kuwa wanakwenda kukutana na timu rahisi. Js Saoura wamebadilika kuanzia kwenye benchi la ufundi lilokuja Dareslaam mpaka kwenye mbinu za kiufundi na wachezaji. Na ili simba kufanya vizuri katika mechi hiyo basi kwanza wachezaji wa Simba wanatakiwa kisaikolojia kuzichukua kelele za mashabiki wa Js Saoura na kuzigeuza kuwa kelele za mashabiki wao katika uwanja wa Taifa pale Dareslaam na hasa siku wakicheza na Alahaly. Kwenye mechi na Js Saoura wachezaji wa Simba wanatakiwa kujituma kwa ushirikiakiano kama walivyojituma kwenye mechi na Ahaly au zaidi wakati walipocheza nao pale Dar. Wachezaji wa Simba wanatakiwa kuwa makini ikiwezekana man to man na wachezaji wa Soura from the start of the game kwakuwa wao ndio wanaotakiwa kujilinda zaidi kwa tahadhari kwani ndio wapo ugenini. Vile vile Simba wanatakiwa kuwa na mikakati maalum katika eneo lao la kiungo kwani kama siri moja kubwa waliokuwa nao Js Saoura ya kuimaliza Simba mapema basi ni kwenda kulifanya eneo la kiungo la Simba kuwa useless au halina msaada wowote katika kuiunganusha timu kwani Soura wakiangalia tu mechi ya Simba na Yanga na wakiongezea na maufundi yao basi watakuwa wameshamaliza kazi ya kuiua Simba.kwa hivyo Simba wanatakiwa kuwaweka sawa zaidi wachezaji wao kiungo kuelekea mechi na Js Saoura kwani katika eneo hilo ndipo mechi yenyewe itakapoamuliwa.
ReplyDelete