March 4, 2019



KOCHA wa Mbao FC, Ally Bushiri amesema kuwa kikosi chake kinapozwa na umakini wa washambuliaji wake kushindwa kumaliza nafasi ambazo wanazitengeneza.

Mbao FC wamepoteza pointi sita mfululizo kwenye ligi baada ya kupoteza nyumbani mbele ya Yanga kwa kufungwa mabao 2-1 kisha jana kupoteza mbele ya Mtibwa Sugar kwa kufungwa mabao 2-0.

"Uwezo tunao a hakuna ambacho kinatumaliza zaidi ya umakini wa washambuliaji wang kushindwa kumalizai nafasi ambazo wanazitengeneza, ushindani ni mkubwa ila bado tuna nafasi ya kufanya vizuri katika michezo yetu inayofuata," amesema Bushiri.

Mbao FC imecheza michezo 28 imeshinda michezo 9 sare 9 na imepoteza michezo 10 ikiwa na pointi 36 kibindoni ikiwa nafasi ya sita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic