March 4, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa licha ya kupata ushindi mbele ya Alliance FC bado wachezaji wake walicheza chini ya kiwango hali iliyowafanya wapate taabu kupata ushindi.

Zahera amesema kuwa mchezaji wake Heritier Makambo aliufanya mchezo uwe mgumu kwani alipanga mapema kabisa kuumaliza mchezo kabla ya kipindi cha pili.

"Makambo alikosa penalti kipindi cha kwanza hali iliyofanya tuanze upya kuutafuta ushindi, pongezi kubwa kwa Amiss Tambwe kwani alitimiza kwa wakati maelekezo ambayo nilimpa.

"Niliamua kumtoa Boban na Ngasa baada ya kuona wapinzani wetu ni watu wa spidi na nikagundua kwamba udhaifu wao ni kujisahau hasa wakienda kushambulia wanakwenda wote wanachelewa kujilinda hilo ndio kosa lao na nilipowafunga nilibadilisha mfumo, nikatumia 5:3:2  na tulianza na 4:4:2," amesema Zahera.

Tambwe alifunga bao dakika ya 75 na kuifanya Yanga kujikita kileleni wakiwa na pointi 64  baada ya kucheza michezo 26 huku wapinzani wao Simba wakifukuza mwizi kimyakimya kwani wamecheza michezo 20 wana pointi 51.

2 COMMENTS:

  1. Naona lugha za kumkejeli mnyama sasa zinapoteza nguvu yake na kila wakitama nyuma wanakiona kivuli cha mnyama aliechelewa kuonkoka kipo nyuma kinawafata na kuwapa kiwewe

    ReplyDelete
  2. Kocha jaribu kupunguza media coverage watanzania ni wapotoshaji sana wanaweza wakazua uongo out of your words....Ndio kuna njia sahihi za kuhimiza michango lakini kuweka wazi katika media hizi....kwani maadui watataka kutumia mwanya huu kuwavuruga wakati ligi bado inaendelea....na ukawashusha morali wachezaji.....Hii ni mbinu ya maadui kutaka kuwavuruga Yanga....kwahiyo Kocha usiwape nafasi hii...kwa kuwashurutisha wanachama wa Yanga wachangie...au la sivyo unasema utaiacha timu.....kuna sababu kwanini zoezi lina muitikio mdogo mojawapo Yanga hawana uongozi wa kuchaguliwa....uchaguzi wao umeingiliwa na TFF na Serikali na baadhi ya wanachama wasio waaminifu wakitumiwa na maadui kwahiyo ndio maana michango haiendi kama kocha unavyotaka....lakini uchaguzi ukifanyika mambo yatabadilika....kwahiyo kocha Zahera inabidi ashauriwe kwa busara katika hili....asiwape nafasi maadui kwa kwenda kwenye media na kusema kama wanachama na mashabiki wa Yanga hawataitikia kuchanga kwamba yeye ataicha timu....hiki ni kipindi cha kutulia na kuhamasisha uchaguzi...wanachama na mashabiki wa Yanga wawe kitu kimoja!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic