FT: JS Saoura 2- 0 Simba
Uwanja wa Stade 20 Aout 1995 Bechar.
Dakika 90 zimekamilika ngoma inaongezwa dakika moja tu
Mpaka sasa JS Saora wamepiga jumla ya mashuti 17 kwenda langoni huku Simba wakiwa wamepiga mashuti 5.
Dakika ya 88 Kagere anaotea na dakika zinazidi kumeguka kwa mnyama.
Dakika ya 86 kwa sasa milango kwa Simba ni migumu
Jonas Mkude anazidiwa ujanja leo anatoka nje anachukua nafasi Mzamiru Yasin dakika ya 84.
Mtanzania Thomas Ulimwengu huyo anaingia sasa akichukua nafasi ya Z. Hammar na shuti lake la kwanza anakutana nalo Manula.
Dakika ya 79 ngoma bado ng'afu kwa Simba.
Mambo magumu kwa mwamba wa Lusaka, dakika ya 72 anatolewa nje nafasi yake inachukuliwa na Rashi Juma.
Dakika ya 65 Jonas Mkude wa Simba anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu mchezaji wa JS Saoura.
Kwa sasa mpira ni dakika ya 63 Simba wanaonekana wamezidiwa ujanja leo kila idara, JS Saoura wanacheza wanavyotaka kwa sasa, hali ya hewa inaonekana ni tatizo kwao kwa sasa.
Dakika ya 58 Meddie Kagere anaongeza idadi ya shot off Target na kufanya zifikie 3 kwa sasa huku JS Saoura wakiwa wamefany hivyo mara 15.
Dakika ya 51 Mohamedd El Amine Hammia anapachika bao la pili kwa JS Saoura kwa mkwaju wa penalti.
Wachezaji wa Simba bado hawajarejea kwenye ubora wao mipira miguuni kwa wachezaji haikai, kwani mpaka sasa wameto pasi kwa usahihi asilimia 70 huku JS Saoura wakiwa na asilimia 80.
JS Saoura wanatumia mfumo wa 4-1-4-1 huku Simba wakitumia mfum wa 4-4-2.
Hassan Dilunga anatoka nje dakika ya 45 anaingia Haruna Niyonzima .
Mapumziko kwa sasa
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakamilika, Simba wanawenda mapumziko wakiwa wameloa kwa kufungwa bao 1 huku wao wakiwa hawajaambulia bao.
Simba wameotea mara moja kipindi cha kwanza huku JS Saoura wakiwa hawajaotea.
JS Soura umiliki wa mpira ni asilia 58 huku Simba ikiwa ni asilimia 42 kipindi cha kwanza.
JS Saoura wamepiga jumla ya mashuti 12 huku Simba wakiwa wamepiga mashiti 2 kuelekea langoni.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimeongezwa dakika 2 kabla ya kwenda mapumziko.
Dakika ya 40 kwa sasa bado Simba hawajaona lango la JS Saoura ikiwa ni bado dakika tano kukamilika kipindi cha kwanza.
Beki ya JS Saoura ina utulivu wa hali ya juu na inaanzisha mashambulizi kwenda kwa Manula, kwa upande wa Simba mzigo mzito kwa Wawa akisaidiana na Bukaba ambaye bado hajaelewa vizuri afanye nini.
JS Saoura wamepiga kona 5 huku Simba wakipiga kona 1 pekee.
JS Saoura wamecheza faulo 2 huku Simba wakiwa wamecheza faulo 5 dakika ya 31.
JS Saoura wamepiga shot on target 3 huku Simba wakiwa hawajapiga shoton target hata moja mpaka sasa dakika ya 29.
Mchezo kati ya JS Saoura unaendelea kwa sasa nchini Algeria dhidi ya Simba ikiwa ni hatua ya makundi.
Simba
.
JS Saoura wanatangulia mbele kwa kumtungua Aishi Manula dakika ya 18 nje ya 18 na mpira ukazama nani ya nyavu kupitia kwa Sid Ali.
Ushindani ni mkubwa huku wachezaji wa Simba wakishindwa kupata utulivu ndani ya Uwanja kwa sasa.
umuhimu wa okwi umeonekana
ReplyDelete