MCHEZO wa Ligi ya hatua ya makundi kati ya JS Saoura na Simba ya Tanzania ngoma imekuwa ngumu kwa wawakilishi kutoka Tanzania ambapo wamekubali kichapo cha mabao 2-0.
Mchezo wa leo Simba walikuwa wamepoteana tangu kipindi cha kwanza ambapo kila mchezaji alicheza kama yupo Ligi Kuu Bara hali iliyowapa nafasi wapinzani wao JS Saoura kuwashambulia na kupata bao la kwanza dakika ya 18 ambalo lilidumu mpaka mapumziko.
Ngoma iliporudi kipindi cha pili wachezaji wa Simba wakajisahau tena na kuendelea kuutafuta mpira kama ni mchezo wa kirafiki huku wakishindwa kumiliki mipira mguuni.
Dakika ya 51 msumari wa pili ulikomelewa na kuwafanya Simba wasiwe na ujanja zaidi ya kuchezewa nusu Uwanja, pia hata namna walivyokuwa wakifanya mashambulizi ilikuwa ngumu kupindua meza.
Kwani kwa muda wa dakika 90 Simba wamepiga jumla ya mashuti yasiyolega lango sita huku JS Saoura wakipiga mashuti 18 yasiyolenga lango.
Matokeo hayo yanaipa ugumu Simba kupenya kimataifa hatua ya robo fainali kutokana na milango kuwa migumu hasa kundi D ambalo kocha wa Simba Patrick Aussems alisema lipo wazi.
Kwa sasa kundi D lipo namna hii:-
JS Saoura ambaye alikuwa anaburuza mkia dakika kadhaa akiwa na pointi tano ndo kinara akiwa na pointi 8 baada ya kuinyoosha Simba mabao 2-0.
Al Ahly anabaki na pointi zake saba akiwa nafasi ya pili baada ya kunyooshwa leo na AS Vita.
AS Vita mbabe wa Simba anamshusha mpaka nafasi ya nne akiwa na pointi saba baada ya kumyoosha Al Ahly leo bao 1-0.
Mwakilishi pekee Simba kutoka nafasi ya tatu anashushwa kishkaji na kibabe na JS Saoura ambaye kwa sasa ni kinara wa kundi D, Simba anabaki na pointi zake sita alizotoka nazo Dar es Salaam.
Simba kupenya hatua ya robo fainali kwa sasa ni neema tu ya Mungu na maajabu ya mpira tusubiri na tuone kwani bado wana mchezo mmoja mkononi kama ambavyo Ofisa Habari wa Simba Haji Manara alisema awali.
Maajabu ya vipi?
ReplyDeleteWacha unazi. Simba akishinda kwa ushindi wowote nyumbani ameingia robo fainali.Na kama iliwezekana kwa Al ahly na Saoura inawezekana wakashinda. Hakuna cha maajabu wala nini.
HUYU KWELI HAJUI MPIRA WALA HAJUI UCHAMBUZI. SIMBA AKIIFUNGA VITA KWENYE MCHEZO WAO UJAO ANAINGIA ROBO FAINALI MAANA ATAKUWA NA POINTI 9 AMBAZO ZITAKUWA ZIMEMVUSHA KUCHUKUA MOJA YA NAFASI 2 ZA JUU ZA MSIMAMO WA KUNDI D.
ReplyDeletemwandishi acha unazi
ReplyDeletemwandishi unateseka sana na Simba na bado utateseka zaidi ya sasa unavyoteseka.
ReplyDeleteWaandishi wa saleh jembe wana unazi sana !kama hujui timu ambazo zitachezea nyumbani mechi ya mwisho ndiyo zitafuzu.utateseka sana
ReplyDelete