March 28, 2019


TIMU ya JKT Queens imedhihirisha kwamba ni moto wa kuotea mbali baada ya kucheza michezo 14 bila kupoteza hata mmoja huku uongozi ukisistiza unahitaji kutetea kombe lao.

JKT Queens ambao wanashiriki ligi ya wanawake maarufu kama Serengeti Lite Women's League ni vinara kwa sasa kwenye ligi wakiwa wamejikusanyia pointi 42.

Kocha mkuu, Ally Ally amesema kuwa uzoefu wa ligi pamoja na wachezaji kujituma unawapa matokeo chanya kwenye michezo yao wanayocheza.

"Ligi ni ngumu na ushindani ni mkubwa ila kinachonisaidia ni uzoefu pamoja na juhudi za wachezaji uwanjani hali hii inanipa matumaini ya kutetea kombe letu msimu huu.

"Hakuna kitu chepesi kwani kila timu ambayo tunacheza nayo inakaza ili kuvunja rekodi ila inakwama kutokana na maandalizi na mbinu ambazo ninawapa wachezaji wangu kila siku, tuna mabao 82 tumefungwa matatu pekee," amesema Ally.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic