KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa kwa sasa mzunguko wa pili mwenendo wa Ligi Kuu Bara umepoteza dira kutokana na waamuzi kutibua mipango ya timu ambayo inajipanga kushindana kihalali.
Lipuli haijawa na matokeo mazuri kwenye mechi zake za hivi karibuni ambapo ilianza kupoteza mbele ya Stand United kabla ya kufungwa na Simba na Kagera Sugar hali ambayo imemkasirisha Matola.
Matola amesema kuwa mzunguko wa kwanza ulikwenda sawa malalamiko yalikuwa kidogo ila kwa sasa kila mwenyeji anamuonea mgeni kibabe.
"Kwa sasa hakuna haki ambayo inatendeka kwenye mpira dhuluma za wazi zinatendeka huku waamuzi wakitazama bila kuchukua hatua, hili ni jambo la hatari ambalo linapoteza utamu wa ligi.
"Waamuzi wanaminya sheria 17 bila sababu hasa ukiwa mgeni unaonewa sana, mechi zote za ugenini zijafungwa kihalali, kwa michezo ambayo haionyeshwi na Azam TV kunamadudu makubwa yanajificha," amesema Matola.
Mwenyekiti wa Chama Cha waamuzi Tanzania, Salum Chama amesema kuwa kwa waamuzi ambao wanakiuka kufuata sheria 17 za mpira hupewa adhabu ikibainika kama wamehusika kutenda makosa ya wazi.
Kuna timu pendwa inaandaliwa ubingwa
ReplyDeleteMatola wakikuckia wazazi wa motto pendwa utalimwa mwaka mmoja jela na mchango wa haruxi utachangia kwa lazma