March 7, 2019


Nahodha wa zamani wa Serengeti Boys, Ally Msengi amepata nafasi ya kufanya majaribio katika moja ya timu kubwa nchini Ufaransa.

Msengi anatarajia kwenda kujiunga na Lille ya nchini Ufaransa kwa ajili ya kufanya majaribio.

Akizungumza na SALEHEJEMBE, wakala maarufu wa wachezaji, Paul Michell kutoka kampuni ya Siyavuma ya nchini Afrika Kusini amesema tayari kila kitu kwa Msengi kimeenda vizuri.

“Kila kitu kimekwenda vizuri na sasa kuna mambo kadhaa ya kumalizia kabla ya yeye kuanza safari,” alisema.
Kwa sasa Msengi anakipiga katika kikosi cha KMC cha Kinondoni jijini Dar es Salaam.


Wakati akiwa chini ya umri wa miaka 17, Msengi alikuwa nahodha wa Serengeti Boys iliyokuwa inashiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, kipa namba moja akiwa ni Ramadhani Kabwili ambaye sasa ni kipa namba moja wa Yanga.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic