March 5, 2019


SIMBA leo Jumanne, wanafanya safari ya kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya wenyeji wao, JS Saoura.

Hata hivyo, kuna hatihati kubwa mshambuliaji wa timu hiyo, Mganda Emmanuel Okwi asiambatane na timu hiyo nchini humo kutokana na hali yake ya kiafya kutokuwa sawa.

Imebainika kuwa Okwi anasumbuliwa na goti ambalo aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli FC, Jumanne iliyopita na kushindwa kuambatana na timu yake hiyo mkoani Shinyanga, kwa ajili ya mchezo wa jana wa ligi kuu dhidi ya Stand United.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba ambazo Championi Jumatatu limezipata zimedai kuwa tatizo hilo ndilo hasa lilimfanya kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems amrudishe jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.

“Siyo kwamba Okwi alirudishwa Dar kwa sababu ya jeraha aliloumia chini ya jicho katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam FC ila ni baada ya kuumia goti katika mchezo wetu na Lipuli.

“Kwa hiyo, kuna hatihati asisafiri na timu kwenda Algeria, kama hatakuwa vizuri ila jibu kamili tutalipata kesho (jana) baada ya timu kutoka Shinyanga,” kilisema chanzo hicho cha habari. Alipotafutwa Okwi ili aweze kuzungumzia suala hilo, hakupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuita tu bila ya kupokelewa.

Hata hivyo, Daktari wa Simba, Yassin Gembe alipoulizwa kuhusiana na hali ya Okwi alisema: “Maendeleo yake ni mazuri ila kuhusiana na kusafiri siwezi kusema kama atasafiri au hatasafiri, sababu bado kuna muda kidogo kabla ya safari hiyo, kwa hiyo siwezi sema chochote kwa sasa.”

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic