March 5, 2019


Wateja 15 wa DStv wameibuka washindi wa wiki ya kwanza ya promosheni ya “Tia kitu pata vituz” inayoendeshwa na MultiChoice Tanzania.

 Kampeni hiyo itakayodumu kwa wiki 8, itakuwa ikitoa washindi 15 kila wiki hivyo jumla ya washindi 120 katika kipindi chote cha promosheni watapatikana.
  
Promosheni hiyo ni kwa wateja wote wa DStv ambao watalipia vifurushi vyao kabla havijakatika.

Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shekulindo amesema “Mteja yeyote wa DStv atakayelipia kifurushi chake kabla hakijakatika moja kwa moja anaingia katika droo na ana fursa ya kujishindia kifurushi chake kwa muda wa miezi miwili”.

Akizumgumza baada ya kujuzwa kuhusu ushindi wake huo Neema Nsabimana ambaye ni mteja wa DStv aliyepo mkoani Mwanza amesema kuwa amefurahi sana kuibuka mshindi kwani yeye ni mpenzi wa vipindi vya DStv hivyo waendelee kuwajali wateja wake hivyo hivyo.

Naye Lulu Mahamba wa Dar es Salaam, amefurahishwa na zawadi hiyo na kueleza kuwa kweli DStv inawakumbuka wateja wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic