March 19, 2019


KOCHA wa timu ya Simba, Patrick Aussems amesema kuwa uwezo wa kikosi chake unaendelea kukua kila siku hasa baada ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba leo wameibuka kidedea mbele ya Ruvu Shooting kwa ushindi wa mabao 2-0 ambayo yamefungwa kipindi cha pili kupitia kwa Paul Bukaba dk ya 52 na Meddie Kagere dk 56 kwa mkwaju wa penalti.

"Tunapambana kufanya vizuri kwa kuwa tuna mashindano makubwa ambayo tunakwenda kushiriki bado tuna kazi ngumu ya kufanya ila imani yangu kila kitu kitakuwa sawa," amesema Aussems.

Kocha wa Ruvu Shooting, Abdulmutik Haji amesema kuwa wameshindwa kupata matokeo licha ya kutengeneza nafasi nyingi walizopata.

"Tumetengeneza nafasi nyingi tumeshindwa kuzitumia ila bado tuna nafasi ya kufanya vizuri, bado kuna matatizo kwa waamuzi," amesema.

Ushindi huo unakuja baada ya kupenya hatua ya robo fainali baada ya kuitungua AS Vita mabao 2-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic