March 19, 2019





Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo kimeendelea na mazoezi kuiwinda Uganda Kwa ajili ya mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Afrika Afcon 2019.

Michuano ya Afcon imepangwa kufanyika nchini Misri Juni, mwaka huu.




Mazoezi hayo yamefanywa Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam chini ya kocha Mkuu  Emmanuel Amunike.

Wachezaji kadhaa wanaocheza soka nje ya Tanzania wakiongozwa na nahodha msaidizi Himid Mao, Thomas Ulimwengu, Saimon Msuva, Rashid Mandawa, Hassan Kessy na wengine wameungana na wenzao wanaokipiga hapa nyumbani.



Nahodha Mbwana Samatta atajiunga kesho na kikosi Leo alipewa mapumziko maalum baada ya kutua nchini usiku wa kuamkia leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic