NAHODHA Msaidizi wa Simba, Mohamed Hussen 'Tshabalala' amesema leo wana kazi ngumu kupata matokeo ugenini kutokana na ushindani uliopo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tshabalala amesema kwa sasa hesabu za kila mchezaji ni kuona namna gani atapambana kutimiza jukumu lake la kuipa timu matokeo kwa kushirikiana ili kutimiza malengo ya timu.
"Sisi sote ni timu moja na kila mchezaji ana morali ya kupambana kupata matokeo kwa ajili ya timu, ni wajibu wetu kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa leo.
"Tupo ugenini hilo lipo wazi ila haina maana tutashindwa hapana, uwezo tunao na nia tunayo ni suala la muda tu mashabiki watuombee ili tufanye vizuri nasi Uwanjani tutapambana," amesema Tshabalala.
Simba itamenyana leo na JS Saoura ya Algeria mchezo wa hatua ya makundi ikiwa ni marudiano, mchezo wa kwanza Simba ilishinda mabao 3-0 Uwanja wa Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment