MENEJA wa Machester United, Ole Gunnar Solskjaer ameshangwaza na kitendo cha picha yake kutumika kwenye matangazo ya kampuni zinazoendesha michezo ya kubashiri bila kibali chake.
Solskjaer amesema kuwa suala hilo amelikabidhi mikononi mwa mwanasheria wake baada ya kutambua kwamba imetumika bila ruhusa katika matangazo hayo.
"Kama kutatokea jambo lolote ambalo mimi nitatakiwa kufanya kwa sasa sina juu ya hii kampuni ya michezo ya kubashiri, hivyo nina hofu kama inaweza kutokea tatizo kwangu hapo baadaye, kitu ambacho nitakisimamia ni kuliacha suala hili kwa mwanasheria ambaye atakwenda kulitazama ni namna gani atalishughulikia kwa ukaribu.
Mwanasheria wa Solskjaer's, Erik Flagan amesema "Hili suala sio jepesi kwani wengi wamekuwa wakitumia picha ya Solskjaer pamoja na jina bila makubaliano, hivyo nashauri kama kuna kampuni inahitaji kufanya biashara kwa kutumia jina lake lazima tuketi tuzungumze,".
0 COMMENTS:
Post a Comment