March 2, 2019


HUKU moto wao kwenye ligi kuu ukiwa haupoi kwa sasa, Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wamewatuma mashushu mapema ili kuandaa mazingira kabla ya timu kukwea pipa kuwafuata waarabu hao.

Simba watamenyana na JS Saoura ya Algeria machi 9 mwaka ikiwa ni mchezo wa marudio kwao huku mchezo wao wa awali uliochezwa uwanja wa Taifa walizindua kampeni yao ya Yes we Can kwa ushindi wa mabao matatu.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mwenyekiti wa Simba, Sued Mkwabi amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo huo na namna ambavyo wanapaswa wapeperushe bendera kimataifa hali iliyowafanya watume watu mapema kwenda kuweka mambo sawa.

"Kwa sasa tayari kuna watu ambao tumewatuma Algeria ili wakaandae mazingira ya timu kabla ya sisi kwenda jumla," alisema kwa kifupi Mkwabi.

Simba wanahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili kujiweka kwenye mazingira mazuri katika kundi D ambalo kwa sasa wanashika nafasi ya pili wakiwa na ponti sita wakifuatiwa na wapinzani wake JS Saoura wenye pointi tano nafasi ya tatu huku Al Ahly wakiwa ni vinara wana pointi saba, AS Vita wanapointi nne nafasi ya mwisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic