March 16, 2019


Kumekuwa na malalamiko ya Kocha Mwinyi Zahera kwamba aliaga anarejea kwao DR Congo katika majukumu ya timu ya faida.

Akaicha Yanga ikisafiri kwenda katika majukumu dhidi ya Lipuli FC mjini Iringa.

Baadaye ametuhumiwa kuendelea kubaki jijini Dar es Salaam kuisaidia AS Vita inayofundishwa na rafiki yake Ibenge ili iimalize Simba kwenye mechi ya mwisho hatua ya makundi kwenda robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

KAMA NI KWELI Zahera kafanya hivyo ni kosa maana atakuwa si mkweli kwa Wanayanga lakini atabaki kuwa sehemu wa shujaa wa taifa lake kama Vita Club itasonga mbele au la.

Maana Zahera achana na urafiki na bosi wake Ibenge lakini atakuwa MTAIFA na anajua faida ya Vita Club kusonga mbele kwa DRC. Zahera ANALAUMIWA sawa lakini ANATUFUNDISHA.

JITAFAKARI wewe Mtanzania unayetaka kufa kwa jazba, presha eti Vita Club ya DR Congo?

Jifunze kwa Zahera ambaye angeweza kujivunia Simba inatoka Tanzania eneo analofanyia kazi na anaishi na Watanzania walio Yanga na Simba. SEMBUSE WEWE hupajui Congo wala hakuna anayejukujua kule unataka KUONYESHA una machunguuuuuu.

Si lazima kuishabikia timu Ila jifunze unatakiwa kufanya hata kama huelewi kabisa linapofikia suala la UTAIFA.

Na Saleh Ally

9 COMMENTS:

  1. Kabisa brother Saleh umenena kineno cha maana kiclicokwenda uvunguni mwa mioyo ya watanzania wengi uliposindikwa ujinga wetu huku tikijifanya werevu. Watanzania hatuna uzalendo na ni moja ya mambo yanayotughrimu kusonga mbele kimaendeleo na kuyapeleka maendeleo kwa wenzetu huku tukijitengenezea mazingira ya kuonekana kuwa watu hovyo. Kuhusu kama kweli Zahera anaisaidia As vita kuifunga Simba? Sijui ushahidi gani tena unaotakikana kwani alijitahidi kufanya hivyo kwa siri katika mechi iliyopita lakini hivi sasa anafanya kwa dhahiri. Zahera anayafanya anayoyayafanya sasa kwakuwa ameshajua watanzania ni wa hovyo linapokuja suala la uzalendo. Zahera wala hajali kama Simba itasonga mbele katika hatua nyengine kuna uwezekano mkubwa wa Yanga yake ikabebewa kushirki klabu bingwa Africa.

    ReplyDelete
  2. Zahera kashagundua akili zetu ziko wapi ndipo akaona haitakuwa ajabu yy kufanya dhahir shahir haya ya kuisapoti VITA. #MUNGU IBARIKICTZ #MUNGU IBARIKI SIMBASC.

    ReplyDelete
  3. Zahera kashagundua akili zetu ziko wapi ndipo akaona haitakuwa ajabu yy kufanya dhahir shahir haya ya kuisapoti VITA. #MUNGU IBARIKICTZ #MUNGU IBARIKI SIMBASC.

    ReplyDelete
  4. Ntajie taifa duniani ambalo club zake zinaonyesh uzalendo....juzi t pep guardiola alisem anataman Bayern Munich ipite japo yupo EPL Na Liverpool...rivals hazitakuj futika dunian.Muhim Leo ni ushind atoe siri, awe hata kwa bench km Koch msaidiz ss hatujal tunatak 3 point basi.....

    ReplyDelete
  5. Ungeanza kuwaambia simba kwa miaka minne wameshavaa jezi za timu ngapi za nje ili kuzisapoti dhidi ya yanga...unadhani yanga walikuwa hawaumii na ukosefu huo wa uzalendo!!?? Acha unafiki ikiwa wewe ni simba usilazimishe yanga wawe simba...manji aliwaingiza mashabiki bute dhidi ya tp mazembe ili kuipa yanga sapoti lkn mikia nyinyi mliishia kuizomea na kuishangilia tp mazembe muda wote....ushamba gani huu wa kuzuia basi ili kumsaka Mwinyi zahera ina maana simba inamuogopa sana?

    ReplyDelete
  6. zahera ayuko sahihi, vp km vita angecheza dhidi ya yanga?? kwa maana angelobb matokeo kisa uzalendo??
    Kosa lake ni kuiacha yanga ikienda lipuli ilihali y hana excuse ya kiafya,kifamily,

    ReplyDelete
  7. Kwa mini tunajitaabisha? Au tunaanza kujenga hoja kuhalalisha kufungwa kwetu? Kwa ni nani alivujisha siri za timu yetu Kyle Algeria? Tujiamini na timu yetu, au tulimtegemea Zahera aje mazoezi ya Simba? Tusijipotoshe kwa hofu zetu, kila timu inatafuta matokeo

    ReplyDelete
  8. Kuna mjinga ametoa mfano wa Guardiola.Kweli unafikiri Guardiola angeiacha Manchester City na kwenda kuisaidia Bayern??
    Ujinga ni ujinga hata ukifanywa na kocha wetu.
    Ni kosa kubwa kuiacha timu yetu ili aisaidie As Vita.
    Sababu aliyoitoa ni ya kijinga eti wanakwenda kufanya matayarisho ya timu ya Taifa?
    Wachezaji karibu wote wanawakalisha klabu zao. Wa As Vita na TP Mazembe.
    Zahera amechagua Taifa lake kwani anajua hakuna anayeweza kumkemea kwani kwenye Yanga yetu5kwa sasa yeye ndio Bodi.Na huu ndio ukweli mchungu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic