March 16, 2019

1 COMMENTS:

  1. Kuelekea michezo wa kesho kati ya Simba na As vita kocha na benchi lao la ufundi la Simba ndio wasimamizi na ni wafanya maamuzi lakini watu wa karibu na kocha lazima wamshike sikio kuwa na macho ya karibu na wachezaji wake wawili ambao kiasi kikubwa Simba inaingia uwanjani kesho ikiwa inawatumainia zaidi kufanya mambo makubwa. As vita ishakuwa na mipango mikubwa iliyotengenezwa hapa nchini na wadau wao ya kuwatoa mchezoni wachezaji hao wawili wa Simba ili kuikata pumzi Simba mapema. Wahezaji hao ni ZANA COULIBALI na CLETUS CHOTA CHAMA. Moja ya mikakati ya As vita ni kuwatoa mchezoni wachezaji hao wawili from the start of game. Suala jengine Simba katika mechi iliyopita na As vita waliambiwa zaidi ya mara laki moja kuwa makini na baadhi ya wachezaji wa As vita lakini kilichotokea ni ujinga mtupu kule Kinshasa kwani wachezaji wale wale walioelekezwa Simba kuwa nao makini ndio walioiadhiri Simba. kama kwenye mechi ya Simba na Nkana ya Zambia jinsi Simba walivyotahadharishwa kuwa makini na Bwalya matokeo yake ni Bwalya huyo huyo aliekaribia kuifungisha virago Simba kwenye klabu bingwa. Wachezaji wa Simba uwezo wanao kama wataamua kujitoa kesho tatizo la Simba ni kutokuwa makini na kutokutulia katika dakika za mwanzo za mchezo. Tatizo hili ni la muda mrefu kwa Simba kuanzia mechi ya Elmasry ya Egypt Simba waliporuhusu mabao mawili ya mapema hapa nyumbani na mabao hayo mawili ya mapema ndio yaliyokatisha safari ya Simba mapema kwenye caf confederation cup. Kwa hivyo kwa kiasi fulani tatizo ni kwa wachezaji wenyewe kuonekana kutokuwa tayari kukabiliana na dhuruba ya mchezo kama wanavyotarajiwa. Labda ni udhaifu wa wachezaji wa kitanzania kuwa na tabia ya kuonekana kusinzia mwanzoni mwa mchezo na kwa kutambua hivyo labda ndio maana timu za nje zimekuwa zikitumia muda huo kuzimaliza timu zetu mapema. Sasa Wachezaji wa Simba kesho pale Taifa lazima wajue hilo tatizo lipo la kujisahau sahau uwanjani na tabia ya kukabia macho badala ya kumkaba mchezaji pinzani inavyotakikana. Nafasi wanayo Simba nafasi kama hizi huwa haziji mara kwa mara,sasa inapotkezea ni vizuri kutofanya makosa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic