Na Saleh Ally, Antalya
Mshambuliaji nyota wa kikosi cha timu ya taifa ya vijana, Serengeti Boys, Kelvin John ameivutia klabu ya Ajax ya Uholanzi.
Ajax imetangaza nia ya kumchukua Kelvin na wakala, Paul Michell amesema ataondoka mara tu baada ya michuano ya Afcon.
Akizungumza na SALEHJEMBE hapa mjini Antalya, Michell amesema Kelvin anaweza kupelekwa klabu ya Ajax Cape Town ya Afrika Kusini au kwenda moja kwa moja nchini Uholanzi na tayari mazungumzo na wasimamizi wake, yameanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment