March 7, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera amemtaja mwenyekiti mpya anayehitajika kuiongoza klabu hiyo. Hiyo ikiwa ni siku moja tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litangaze Machi 24, mwaka huu ndiyo siku ya uchaguzi huo.

Awali, uchaguzi huo ulisimamishwa na TFF baada ya kuzuiwa mahakamani na baadhi ya wanachama. Zahera alisema, mwenyekiti huyo anatakiwa awe na mipango thabiti ya kutafuta vyanzo vya mapato kupitia makampuni mbalimbali.

“Wanachama nawasikiliza wenyewe kila siku wanataka uchaguzi ufanyike, lakini shida inakuja wapo hao viongozi watakaoingoza Yanga kwa mafanikio.

“Hao viongozi wanaotaka kuiongoza Yanga, je wanafahamu hali ya kiuchumi iliyokuwepo kwenye timu, ni vema wakalifahamu kabla ya kuingia madarakani. 

“Niwaambie Wanayanga wawe makini katika uchaguzi huo kwa kuweka viongozi watakaoiondoa klabu katika kipindi kigumu cha kiuchumi kwa sababu Yanga ni klabu kubwa yenye mtaji mkubwa wa mashabiki,” alisema Zahera.

5 COMMENTS:

  1. Sasa this is too much mpaka inaboa kila siku Mwinyi Zahera...jamani tumechooooooka!!!! Leteni habari mpya

    ReplyDelete
  2. This is too much;kocha sasa aingilia madaraka yeye ni mkongo lakin mpaka sasa vingozi anaowataka yeye huyu ndo zahera, ndo nan haswa

    ReplyDelete
  3. yanga haina msemaji au mbona kilasiku kwasukwasu ndo anaongea dismas ten #shkamoo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Msemaji wa Man U au Man City au Mamelodi au timu yoyote ya nje ushamsikia kwenye media? Zahera yuko sahihi

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic